Nimepitapita mitaani nasikia stori nyingi wazee ambao ni watumishi wakilalamika sana kuhusu kukatwa mafao yao kwa asilimia 75% na kupewa asilimia 25%.Kweli huu mfumo watumishi wengi wameonesha kutouelewa sana wengine wakilalamikia waheshimiwa wabunge ambao wamepitisha sheria hiyo,binafsi naona kwamba mfumo nimeuelewa lakini wapo watakaofaidika nao lakin pia wapo ambao hawatafaidi sana,mfano mstaafu akistaafu akachukua mafao yake ya 25% na kila mwezi akawa anachukua asilimia 75 akiishi zaidi ya miaka 10 baada ya kustaafu ataweza kufaidi kwa kiasi fulan lakin ikitokea Mungu akamchukua mapema habari itakuwa imekwisha hapo hakuna anayepinga wala kujifanya anajikuna .Mimi niwasihi nyie watumishi pigeni kazi kwabidii naamini mambo yatapendeza huko mbeleni .Mungu awape nguvu na uwajibikaji mwema