Mbinu za kuweka akiba
Akiba ni muhimu sana katika harakati za kutafuta maisha,ukizungumza na watu mbalimbali ukawauliza juu ya kuweka akiba utapata majibu mengi,Mwingine atakwambia kwamba "pesa napata lakini haitoshi .Ukijenga utamaduni wa kujiwekea akiba utajikuta pesa yako inatosha.Kuweka akiba sio lazima uwe na kipato kikubwa bali hicho kidogo ukijiwekea mikakati stahiki utaweza kuweka akiba ya kutosha
Hizi no mbinu ambazo kwa namna moja ama nyingine zitakuwwzesha kuweka akiba
1:kuwa na nidhamu ya fedha
Hili ni suala dogo kulifanya lakini ni gumu sana kulitimiza.Fedha yoyote inahitaji nidhamu unatakiwa kuheshimu kila senti unayoipata,epuka matumizi yasiyo ya lazma maana pesa ukiwa nayo itakuongoza kufanya kila jambo maana kwa wakati huo unaona pesa unayo.In bora ukipata pesa weka akiba angalau asilimia kumi kuliko kuitumbua bila mpangilio
2: jiwekee malengo yanayopimika
Watu wengi hasa wa kipato cha kati na cha chini huwa hawajiwekei malengo lakini kuweka malengo kutakusaidia wewe kuweka akiba ya baadae ili kutimiza malengo hayo,mfano umejiwekea malengo kwamba mwakani nahitaji kujenga itakupasa kuzingatia malengo ya kujenga ikibidi weka katika maandishi ili uwe unakumbuka hiyo itakukumbusha kuweka akiba kwa ajili ya kujenga,Malengo ni muhimu Fanya kila jambo kwa malengo.
3:jitenge na kipato chako
Huu ni mtihani sana kwa baadhi ya watu,watu wengi wanashindwa kuishi kama wao wanapenda kuishi kama Fulani,hilo in tatizo ukiishi kama fulani huwezi kuweka akiba maana utafuata malengo ya mwenzako huyo badala ya kuweka na kutimiza malengo yako.Binadamu hatulingani wala hatufanani kwahiyo ishi kama ww tumia kulingana na kipato chako usimuangalie Fulani hapo pesa ya kuweka akiba utaipata
4: jipunguzie kipato kwa asilimia
Jiwekee mikakati kwamba katika kipato chako utakuwa unaweka asilimia kadhaa kwa ajili ya akiba kama ni asilimia kumi au ishirini na ujitahidi kutopindisha maelezo unazingatia kuweka akiba baada ya muda utajikuta una hela mzuri na inakuwezesha kutimiza malengo yako.
5:kaa mbali na kibubu chako
Unapokuwa umeweka akiba kaa mbali nayo sisi bimadamu tumeumbwa na tamaa sana kwahiyo ukipata shida na hela iko karibu na wewe utaitoa tu na uitumie tayari utakuwa umeharibu malengo yako ,hivyo kaa mbali na kibubu chako

Comments
Post a Comment