Hili neno utajiri limekuwa likiwasumbua watu vichwa wanawaza wafanye nn ili kupata utajiri wengine wanadhani kwamba ili kupata utajiri ni mpaka utoe kafara, la si hivyo wala kupata utajiri sio mpaka uingie kwenye chama cha freemason hapana kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu tu na kujitafutia dhambi za bure.Sasa Leo nakudokezea kidogo siri ya utajiri,ukitaka kuwa tajiri itakubidi uanzishe biashara yako ambayo itakuwa na faida ambayo utakuwa na uwezo wa kuimiliki na siyo biashara ikumiliki wewe hapo utakuwa tajiri lakini ukishindwa hilo utaishia kupata pesa ya kula tu.Kama wewe ni mfanyakazi tafuta wazo la biashara anzisha maana hakuna mfanyakazi tajiri duniani matajiri wakubwa ni wafanyabiashara ,hivyo tafakari chukua hatua