Soma hii fact

THAMANI yako HAIPUNGUI kwa sababu watu hawathamini ama kukubali unachofanya.Thamani YAKO inapungua pale ambapo UNAACHA KUFANYA kitu unachojua ni MUHIMU kwa maisha yako na ndicho Kitu SAHIHI kwa kisingizio kuwa WATU HAWAKUTHAMINIHapo unajishushia thamani. Kuna mambo 3 unatakiwa kuzingatia:

1)Kuna watu HAWAKUTHAMINI kwa sababu bado hawajajua thamani yako lakini hiyo haimaanishi wewe hauna thamani. Njia nzuri ya kushinda hili ni kuendelea kufanya kwa ubora wa hali ya juu hadi wanaodhani unabahatisha Wajue kumbe ndio ulivyo.

2)Kuna watu hawakuthamini kwa sababu wanaona unachofanya wanatamani kufanya ila wameshindwa, hivyo wanataka kukukatisha tamaa kwa kukuonyesha kuwa unachofanya hakina thamani.

3)Kuna watu hawakuthamini kwa sababu wanaona haustahili. Duniani kuna maajabu ya watu kufikiri kuwa kuna watu wa aina fulani ndio wanahaki ya kufanikiwa katika mambo fulani. Kama wewe sio mmoja wa kundi hilo, ukianza kufanya wataonyesha kutokukuthamini.Hata Yesu alidharauliwa kutokana na mji aliotoka ulikuwa mdogo-“Hivi jambo JEMA linaweza kutoka NAZARETI”. Walisahau kuwa thamani ya mtu haitokani na UKOO WAKE, ELIMU, KABILA ama MJI anaotoka bali UWEZO ALIONAO. Na wewe “You can Prove them Wrong”.

Kumbuka thamani yako haiongezwi kwa KUBISHANA ama KUSHINDANA na WASIOKUTHAMINI bali kwa KUENDELEA KUFANYA BILA KUCHOKA vitu vya THAMANI.

NAKUKUMBUSHA KUWA WEWE NI WA THAMANI SANA.

Comments

Popular posts from this blog

Mbinu za kuweka akiba

Sifa za biashara inayoweza kufikia mafanikio makubwa