Akiba ni muhimu sana katika harakati za kutafuta maisha,ukizungumza na watu mbalimbali ukawauliza juu ya kuweka akiba utapata majibu mengi,Mwingine atakwambia kwamba "pesa napata lakini haitoshi .Ukijenga utamaduni wa kujiwekea akiba utajikuta pesa yako inatosha.Kuweka akiba sio lazima uwe na kipato kikubwa bali hicho kidogo ukijiwekea mikakati stahiki utaweza kuweka akiba ya kutosha Hizi no mbinu ambazo kwa namna moja ama nyingine zitakuwwzesha kuweka akiba 1:kuwa na nidhamu ya fedha Hili ni suala dogo kulifanya lakini ni gumu sana kulitimiza.Fedha yoyote inahitaji nidhamu unatakiwa kuheshimu kila senti unayoipata,epuka matumizi yasiyo ya lazma maana pesa ukiwa nayo itakuongoza kufanya kila jambo maana kwa wakati huo unaona pesa unayo.In bora ukipata pesa weka akiba angalau asilimia kumi kuliko kuitumbua bila mpangilio 2: jiwekee malengo yanayopimika Watu wengi hasa wa kipato cha kati na cha chini huwa hawajiwekei malengo...
Hili neno utajiri limekuwa likiwasumbua watu vichwa wanawaza wafanye nn ili kupata utajiri wengine wanadhani kwamba ili kupata utajiri ni mpaka utoe kafara, la si hivyo wala kupata utajiri sio mpaka uingie kwenye chama cha freemason hapana kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu tu na kujitafutia dhambi za bure.Sasa Leo nakudokezea kidogo siri ya utajiri,ukitaka kuwa tajiri itakubidi uanzishe biashara yako ambayo itakuwa na faida ambayo utakuwa na uwezo wa kuimiliki na siyo biashara ikumiliki wewe hapo utakuwa tajiri lakini ukishindwa hilo utaishia kupata pesa ya kula tu.Kama wewe ni mfanyakazi tafuta wazo la biashara anzisha maana hakuna mfanyakazi tajiri duniani matajiri wakubwa ni wafanyabiashara ,hivyo tafakari chukua hatua
Comments
Post a Comment