Sifa za biashara inayoweza kufikia mafanikio makubwa
Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa Habarika.com blog nipende kukwambia kwamba kuna biashara nyingi sana duniani.Leo tunazungumzia sifa za biashara inayoweza kukupa mafanikio makubwa.Kimsingi biashara yoyote utakayoamua kufanya kama utakuwa serious nayo ukavumilia na ukajikita hasa inaweza kukulipa lakini kama utaingia kwenye biashara kwa mguu mmoja ( kwa kubeep) bila shaka haitakupa mafanikio mwishowe utakata tamaa ufunge biashara yako.Zifuatazo ni sifa za biashara zenye mafanikio makubwa 1: biashara iwe na urahisi wa kueleweka,ili biashara yako izae mafanikio na kukua zaidi inatakiwa iwe inaeleweka kwa wateja wako na watu wote kwa ujumla kwa urahisi. 2: biashara iwe na wateja wa kujirudiarudia Biashara yoyote yenye watteja wa namna hiyo haiwezi kufa na itazidi kukua kwasababu aliyenunua Jana atarudi leo na kesho na wewe utaendelea kuuza kila siku na kupata faida. 3: Sifa ya tatu ni hii,biashara iwe na bidhaa zisizo...